
Ugonjwa huu huwapata hasa watoto na wazee kutokana na kutokuwa na mfumo imara wa kinga ya mwili . Watu wenye matatizo katika mfumo wa upumuaji kama vile pumu(asthma) wakipata maambukizi hali yao huzidi kuwa mbaya zaidi.
DALILI ZA MTU MWENYE PNEUMONIA
Maambukizi mara nyingi husababishwa na bacteria ambao husababisha dalili zifuatazo
1.Kikohozi kinachoambatana na makohozi mazito ambayo yaweza kuwa na rangi ya kijani au kuambatana na damu.
2.Kuwa na homa .Homa husababishwa na bacteria kutoa kemikali (pyrogens) ambazo huingilia mfumo wa kawaida wa urekebishaji jotoridi la mwili na kufanya mwili kuongeza joto lake ili kuweza kuzuia au kuua vimelea mwilini. Kadiri bacteria walivyowengi mwilini ndivyo jotorid hongezeka na kupelekea homa kali ya mapafu.

4..Maumivu ya kifua .Hali hii hutokea wakati wa kuvuta pumzi ndani au kipindi mgonjwa anapokohoa
5.Kuongezeka kasi ya mapigo ya moyo.Moyo huongeza kasi ya mapigo yake illi kuhakikisha kuwa mwili mzima unapata oxygen kutokana na kupungua ufanisi wa upatikanaji wa oxygen kwa mfumo wa kawaida wa hewa.
ATHARI ZA PNEUMONIA KWENYE MWILI WA BINADAMU
Pneumonia husababisha mwili kushindwa kupata oxygen ya kutosha hivyo kusababisha athari mbalimbali zinazotokana na mwili kupungukiwa oxygen .Mfano wa athari hizo ni kama hypoxemia ambapo kiwango cha oxygen kwenye damu hupungua na kupelekea tishu kushindwa kupata oxygen ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha nishati ya mwili.(hypoxia).
Cyanosis ni tatizo linaloweza kujitokeza ambapo damu ambayo haina oxygen inapokuwa kwa wingi mwilini kuliko yenye oxygen hasa kwa watoto na kumfanya mtoto aonekane kuwa na rangi ya blue . .Hypercabia na hypercapnea ni hali inayotokea ambapo kiwango cha carbondioxide kwenye damu na kwenye tishu huongezeka. Kama maambukizi hayakutibiwa yaweza kusababisha kifo.
NJIA ZA KUJIKINGA NA PNEUMONIA
- Weka mazingira katika hali ya usafi. Hii inapunguza uwezekano wa kuchukua vimelea kutoka sehemu mbalimabli endapo mgojwa wa pneumonia aliyegusa vifaa ambavyo mtu mwingine atatuma
- Usitumie sigara kwani moshi wa sigara hupunguza uwezo wa mapafu kudhibiti vimelea vya pneumonia na hivyo kufanya kuwepo uwezekano wa kuambukizwa pneumonia

3.Chanjo ya pneumonia pia hutolewa ili kujikinga na ugonjwa huu.
2.http://www.m.webmd.com/a-to-z-guides/tc/pneumonia-topic-overview
Prepared by Andrew Luhusa MD Student @ MUHAS
23 Sept 2016
Prepared by Andrew Luhusa MD Student @ MUHAS
23 Sept 2016
No comments:
Post a Comment